array(0) { } Radio Maisha | Wakaazi na viongozi wa Pokot Magharibi watakiwa kuwasilisha hoja Bungeni

Wakaazi na viongozi wa Pokot Magharibi watakiwa kuwasilisha hoja Bungeni

Wakaazi na viongozi wa Pokot Magharibi watakiwa kuwasilisha hoja Bungeni
Wakaazi na  viongozi wa kaunti ya Pokot Magharibi wametakiwa kuwasilisha hoja au lalama zao kuhusu uongozi au changamoto zinazoshuhudiwa kwenye sekta ya afya katika bunge la kaunti ili yaangaziwe na wawakilishi wadi.
 
Akizungumza mjini Makutano spika wa bunge la kaunti hiyo Bi. Catherine Mukenyang amesema kwamba ni kupitia njia hiyo ambapo wawakilishi wadi watajadili maswala yatakalowasilishwa na kuzitafutia ufumbuzi.
 
Wakati uo huo amesema kwamba kuna kamati 21 kwenye bunge ambazo ziko tayari kupokea hoja za wananchi na pia viongozi kisha kuziangazia kwa mujibu wa taratibu za bunge.
 
Aidha amewaonya viongozi dhidi ya kulumbana hadharani huku pia akiwataka kusitisha siasa na kuangazia jinsi ya kuwahudumia wakaazi wa maeneo yao kimaendeleo