array(0) { } Radio Maisha | Washikadau mbalimbali Mombasa watangaza kuendelea na maandamano
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Washikadau mbalimbali Mombasa watangaza kuendelea na maandamano

Washikadau mbalimbali Mombasa watangaza kuendelea na maandamano

Washikadau mbalimbali kwenye Kaunti ya Mombasa wametangaza kutotikisika hadi wakati serikali itasitisha kikamilifu usafirishaji wa makasha ya mizigo kupitia reli ya kisasa SGR.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir amesema kamwe hatoruhusu mpango huo ambao ulitajwa kusitishwa kuendelea kuwaathiri wakazi wa Mombasa na eneo la Pwani kwa ujumla. Kulingana naye kila mshikadau anajukumu la kuendelea kupaza sauti na kutafuta mikakati ya kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa vilivyo.

Hayo yanajiri huku ikiarifiwa kwamba Vuguvugu la Okoa Mombasa litaendelea na maandamo kesho baada ya maandamano ya leo kuahirishwa kufuatia siku ya mapumziko ya madhimisho ya Mashujaa.

Maandamano hayo yameratibiwa kuanza katika bustani ya Uhuru hadi katika jengo la Uhuru na Kazi kuwasilisha waraka mwingine kwa Mshirikishi wa Utawala wa eneo la Pwani John Elungata.

Tayari Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Central jijini Mombasa ameandikiwa barua ya kujulishwa kuhusu maandamano hayo.

IKumbukwe jana mkutano wa maombi wa Vuguvugu hilo ulioratibiwa kufanyika katika Uwanja wa Tononoka ulitibuka baada ya mafisa wa vitengo mbalimbali vya Idara ya Usalama kutumwa kuzuia mpango huo.