array(0) { } Radio Maisha | Kenya Morans ndio mabingwa wa makala ya mwaka huu ya Safari Sevens

Kenya Morans ndio mabingwa wa makala ya mwaka huu ya Safari Sevens

Kenya Morans ndio mabingwa wa makala ya mwaka huu ya Safari Sevens

Kenya Morans ndio mabingwa wa makala ya mwaka huu ya Safari Sevens. Morans ilitawazwa bingwa baada ya kuitandika AfrBlitzebokke ya Afrika Kusini alama 19-14 kwenye fainali. Fainali hiyo iliandaliwa katika uwanja wa Impala RFUEA hapa jijini Nairobi na wachezaji Jeff Oluoch, Geoffrey Okwatch na Alvin Otieno waliisaidia Morans kuizamisha Afrika Kusini.

Tukiachana na Raga tuangazie soka ambapo mabingwa watetezi wa ligi ya KPL Gor Mahia wameendeleza msururu wa matokeo mazuri katika ligi hiyo. Wakicheza ugenini katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru jana Gor Mahia waliitandika Kariobangi Sharks goli 1-0 na kurejea kileleni mwa jedwali la ligi hiyo kwa alama 15. Kocha wa Kariobangi Sharks amewasifia wachezaji wake kwa kuonesha ukakamavu