array(0) { } Radio Maisha | Rais awasihi wafanyakazi wa serikali kuwatumikia Wakenya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Rais awasihi wafanyakazi wa serikali kuwatumikia Wakenya

Rais awasihi wafanyakazi wa serikali kuwatumikia Wakenya

Rais Uhuru Kenyatta amemtuza Mwanariadha Eliud Kipchoge tuzo ya The Elder of Golden Heart CGH, huku akiwapongeza wanariadha kwa kuliletea taifa hili sifa katika ngazi za kimataifa. Aidha rais amewasihi wafanyakazi wa serikali kuwatumikia Wakenya ipasavyo ili kufanikisha ndoto za mashujaa waliopigania uhuru.

Akihutubu wakati wa Maadhimisho ya Mashujaa katika Bustani ya Mama Ngina Jijini Mombasa, Rais Kenyatta ametambua juhudi za mashujaa waliochangia katika maendeelo ya taifa hili, na kumtuza mwanariadha Eliud Kipchoge kwa niaba yao.

Kipchoge amepewa tuzo ya The Elder of Golden Heart EGH , kwa rekodi aliyoiweka kwa kukimbia kilomita arubaini na mbili chini ya muda wa saa mbili wakati wa mbio za INEOS 159.

Rais amesema rekodi ya Kipchoge ni dhihirisho kwamba kila mmoja ana uwezo wa kufaulu iwapo atajidiisha hasa kufatia kauli mbiu yake ya No Human is Limited.

Pia rais alimtambua bingwa wa kike katika mbio za Chicago Marathon Brigit Kosgei, pamoja na wanariadha waliofanya Kenya kuwa nambari ya pili bora kwenye mbio za DOHA.

Aidha Rais amezipongeza Idara za Mahakama, Ofisi ya Mkuu Mashtaka ya Umm na Idara ya Upelelezi kwa hatua kubwa iliyopigwa kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Rais amesema anawatambua mahakimu na majaji ambao wanafanya kazi zao bila mwegemeo huku akiwapongeza wapelelezi wanaofanya ujasusi kwa ukakamavu.

Wakati uo huo Rais amewapongeza wanahabari wanaongazia taarifa za ufichuzi na zenye kuelimisha, huku akitambua juhudi za walimu akiwamo Peter Tabichi aliyepewa Tuzo ya Kimataifa ya Mwalimu Bora miezi kadhaa iliyopita.

Aidha Kenyatta amevipongeza vikosi vya Jeshi la Ulinzi kwa kudumisha usalama ndani na kwenye mipaka ya Kenya.

Hata hivyo Rais amewapongeza Wakenya wanaochangia ukuaji wa taifa hili wakiwamo madaktari, wakulima, madereva, wasanii na waigizaji miongoni mwa wengine huku akiwasihi kuendeleza moyo wa uzalendo.

Amesema ushirikiaono wake na Kinara wa ODM Raila Odinga maarufu Handshake, ulilenga kudumisha uzalendo ulioanzishwa na watangulizi wa taifa hili.

Kwa upande wake Raila amesema Handshake inalenga kufanikisha muungano wa mataifa ya Ukanda wa Afrika Mashariki jinsi ilivyokusudiwa na watangulizi wa mataifa hayo wakiwamo Hayati Mzee Jomo Kenyatta na Julius Nyerere.

Naibu wa Rais Dkt. William Ruto alikwepa kuzungumzia suala la BBI licha ya gavana Joho kumtania hadharani akimtaka kutangaza msimamo wake.

Ruto badala yake ametumia hafla hiyo kufafanua mipango ya serikali katika kuangazia ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana akiwashi Wakenya kujiepusha na siasa za uchochezi.

Maadhimisho ya kitaifa ya Sherehe ya hamsini na sita ya Siku ya Mashujaa yalifanyika katika Bustani ya Mama Ngina Jijini Mombasa huku mengine yakifanyika katika kila kaunti.