array(0) { } Radio Maisha | Je, unaifahamu tuzo ya Order of Elder of the Golden Heart?
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Je, unaifahamu tuzo ya Order of Elder of the Golden Heart

Je, unaifahamu tuzo ya Order of Elder of the Golden Heart

Baada ya Rais kumtuza Mwanariadha Eliud Kipchoge tuzo ya Elder of the Order of the Golden Heart of Kenya (E.G.H.) ambayo ni ya juu zaidi baada ya ile ya Chief of the Order of the Golden Heart of Kenya C.G.H. Je, unaifahamu tuzo ya Order of Elder of the Golden Heart 

Tuzo ya Order of Elder of the Golden Heart ni ya juu zaidi miongoni mwa vitengo vinane vya tuzo zinazotolewa na Rais. Katika Order of the Golden Heart aidha kuna vitengo vitatu kutegemea na hadhi ya wanaotuzwa.

Tuzo ya juu zaidi ni Chief of the Order of the Golden Heart of Kenya (C.G.H.) ambayo hutuzwa marais, kando na marais ambao wamekuwa mamlakani nchini wengine waliotuzwa ni  Rais wa Uganda Yoweri Museveni, aliyekuwa Rais wa Liberia  Ellen Johnson Sirleaf na Agha Khan IV miongoni mwa wengine.

Inayofuata ni Elder of the Order of the Golden Heart of Kenya (E.G.H.) ambayo Kipchoge ametuzwa. Tuzo hii hasa ni kwa manaibu wa rais , Maspika, Mawaziri , wake wa marais, wake wa manaibu wa rais, mkuu wa utumishi wa umma na wakuu wa vikosi vya ulinzi. Tangu Kenya kujinyakulia uhuru miaka hamsini na sita iliyopita ni watu mia moja tisini na wanane waliopewa tuzo hii.

Ya mwisho katika kitengo hiki ni Moran of the Order of the Golden Heart of Kenya (M.G.H.) inayotuzwa makamanda wa jeshi la Ulinzi na Inspekta Mkuu wa Polisi.

Kitengo cha pili kikuu ni  Order of the Burning Spear ambacho kimegawanywa kwa vitengo vitatu pia ambavyo ni  Chief of the Order of the Burning Spear (C.B.S.), Elder of the Order of the Burning Spear (E.B.S.) na Moran of the Order of the Burning Spear (M.B.S.).

Wale ambao wamewahi kutuzwa katika kitengo hiki ni Aliyekuwa Msemaji wa Ikulu Manoah Esipisu Mwanhabari Jeff Koinange, na bingwa wa mbio za mita mia na nane David Rudisha.

Tuzo nyingine ni The Order of the Grand Warrior of Kenya, the Distinguished Conduct Order, the Distinguished Service Medal, the Silver Star of Kenya, Head of State's Commendation na The Uhodari Medal.

Katika vitengo hivi Kamati inayosimamia tuzo za rais hupendekeza orodha ya majina wanaostahili kutuzwa.

Kulingana na sheria kuhusu tuzo za kitaifa wanaostahili kupewa tuzo ni watu ambao wameonesha mfano mzuri wa kuigwa, uzalendo na uongozi, wengine ni waliochangia kwa njia moja au nyingine katika ukuaji wa uchumi, sayansi, elimu, spoti, uanahabari, biashara, usalama miongoni mwa masuala mengine.