array(0) { } Radio Maisha | Ruto asisitiza kwa wananchi ndiyo watakaoamua kuhusu BBI

Ruto asisitiza kwa wananchi ndiyo watakaoamua kuhusu BBI

Ruto asisitiza kwa wananchi ndiyo watakaoamua kuhusu BBI

Huku Mjadala kuhusu Jopo la Upatanisho la BBI ukiendelea Naibu wa Rais William Ruto amesema ni wananchi tu watakaoamua kuhusu mapendekezo yatakayotolewa na jopo hilo. Ruto ameunga mkono Kauli ya rais kwamba ripoti ya Jopo la BBI inastahili kutumika kuwaunganisha Wakenya na kuelta utangamano nchini.

Akizungumza katika eneo la Keiyo Kusini, Kaunti ya Elgeyo Marakwet Naubu Rais hata hivyo, ameendelea kuwasuta wale anaodai kuwa wanalenga kuitimia kujinufaisha kisiasa.

Wakati uo huo Ruto ameendelea kusisitiza kwamba lengo la serikali ya Jubilee ni kuhakikisha kuwa kuna utangamano nchini, na kutokomeza kabisa migawanyiko miongoni mwa Wakenya.

Hata hivyo wandani wa Naibu Rais wameendeelea kulipinga kulipinga jopo la BBI wakisiitiza kwamaba linalenga kuwatafutia watu wachache nafasi za uongozi licha ya Rais Uhuru Kenyatta kupinga madai  hayo. Kipchumba Murkomen ni Seneta wa Elgeyo Marakwet.

Madai sawa na hayo yametolewa na Mwakilishi wa Kike wa Kaunti hiyo Jane Chebaibai.

Ikumbukwe Rais Uhuru Kenyatta ameyapinga madai kuwa Jopo la Upatanishi BBI halilengi kumuongea muda wa kuendelea kuhudumu wala kuongeza nafasi za viongozi serikali badala yake kuhakikisha kuwa kuna kuwapo na umoja na utangamano nchini