array(0) { } Radio Maisha | makundi ya uhalifu yaliyo na nia ya kutatiza sherehe ya Mashujaa yaonywa

makundi ya uhalifu yaliyo na nia ya kutatiza sherehe ya Mashujaa yaonywa

makundi ya uhalifu yaliyo na nia ya kutatiza sherehe ya Mashujaa yaonywa

Mshirikishi wa Utawala eneo la Pwani John Elungata ameyaonya makundi ya uhalifu yaliyo na nia ya kutatiza mshere ya Mashujaa itakayofanyika katika Bustani ya Mama Ngina jijini Mombasa.

Katika taarifa yake, Elungata amesema kwamba mafisa zaidi wa Polisi wametumwa kushika doria kwenye maeneo tofauti ya Pwani ili kuimarisha usalama.

Amewasihi wakazi wa maeneo tofauti ya Pwani kutoa taarifa yoyote ya utovu wa usalama endapo utashuhudiwa.

Elungata kwa mara nyingine amelionya Vuguvugu la Okoa Mombasa linalowajumuisha Wafanyabiashara wa eneo la Pwani ambalo linapanga kufanya mkutano wa maombi kesho kwamba watakabiliwa kwa mjibu wa sheria.

Hayo yanajiri huku usalama ukiwa umeimarishwa kwenye  Bustani ya Mama Ngina ambapo sherehe ya Mashujaa itafanyika