array(0) { } Radio Maisha | Wakenya watikiwa kuwa makini msimu huu wa mvua

Wakenya watikiwa kuwa makini msimu huu wa mvua

Wakenya watikiwa kuwa makini msimu huu wa mvua

Shirika la Msalaba Mwekundu limewashauri Wakenya kuwa makini msimu huu wa mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini. Shirika hilo aidha limewashauri wale wanaoishi kwenye ameneo yaliyo katika athari ya kukumbw ana mafuriko na maporomoko ya ardhi kuhamia maeneo salama. 

Kwenye Kaunti ya Turkana watu zaidi ya elefu 15000 wameachwa bila makao kufuatia mvua kubwa inayonyesha na kusababisha mafuriko. Mike Ekutan anaarifu zaidi.

Wakazi hao hasa wanabiashara mjini Lowdar  wanakadiria hasara baada ya bidhaa zao kusombwa na mafuriko. Joseph Losuru ni mwenyeti wa Muugano wa Soko la mifugo la Lodwar.

Wakazi hawa wamelaumu serikali ya Kaunti ya Turkana kwa kutowapa msaada wa wowote tangu wakabiliwe na janga hilo.

Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Turkana Joyce Emanikor ameyaomba mashirika yasio ya serikali kutoa msaada wa dharura ili kuwaokoa waathiriwa hawa ambao wamewachwa na bila makao.