array(0) { } Radio Maisha | Rais azindua chanjo ya maradhi ya Hpv Mombasa

Rais azindua chanjo ya maradhi ya Hpv Mombasa

Rais azindua chanjo ya maradhi ya Hpv Mombasa

Hatimaye mpango wa Chanjo dhidi ya maradhi ya HPV yanayosababisha saratani ya kizazi imezinduliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta katika shule ya Msingi ya Ziwani jijini Mombasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Kenyatta amesema kwamba hatua hiyo itawezesha kukabiliwa kwa maambukizi mapya ya saratani hiyo kwa watoto wa kike na hivyo kuliwezesha taifa hili kuikabili saratani.

Uhuru amesema kwamba tayatri Wizara ya Afya imebuni mikakati ya kuhakikisha kwamba huduma za ukaguzi na matibabu ya maradhi ya saratani yanafanikishwa katika hospitali zote za Kaunti humu nchini.

Vilevile Rais amesema kuwa ujenzi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta umekamilika na huduma zitaanza mwishoni mwa mwezi huu. Hospitali hiyo inalenga kusaidia pakubwa katika kukabili saratani miongoni mwa wananchi.

Waziri wa Afya Sicily Kariuki kwa upande wake amaetaja umuhimu wa chanjo hiyo, na kusema kuwa uchunguzi dhabiti ulifanywa. Kariuki amesema kwamba chanjo hiyo itarudiwa tena baada ya miezi sita kwa wasichana laki nane ambao wanalengwa kuchanjwa kote nchini.

Gavana wa Mombasa Ali HassanJoho kwa upande wake ameelezea kusikitishwa na wanaopinga mpango huo, wakidai kuwa chanjo hiyo inasababisha matatizo ya ubongo na ulemavu.

Utafiti uliotolewana Shirika la WHO uliobainisha kwamba kuwa kila siku nchini Kenya wanawake tisa hufariki dunia kutoka na saratani ya kizazi.