array(0) { } Radio Maisha | EACC kuendelea kuwazuilia watu sita waliokamatwa

EACC kuendelea kuwazuilia watu sita waliokamatwa

EACC kuendelea kuwazuilia watu sita waliokamatwa

Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC inaendelea kuwazuilia watu sita waliokamatwa mapema Ijuma kwa madai ya kuilaghai ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, EACC imesema kwamba sita hao walidai kuinunulia ofisi hiyo programu ya tarakilishi kwa kima cha shilingi milioni 100.

Aidha, EACC imedokeza kwamba imekuwa ikiendeleza uchunguzi hiyo ikizingatiwa kwamba programu hiyo ilipaswa kuwa shilingi milioni 18 japo sita hao walilipwa zaidi ya shilingi milioni 100.

Stakabadhi za ununuzi zimebainisha kwamba programu hiyo ilinunuliwa kutoka kwa Kampuni ya humu nchini kwa jina Open Systems Integration baada ya kupewa zabuni ambayo haikutangazwa kwa umma.