array(0) { } Radio Maisha | Mitihani ya Kitaifa ya KCPE na KCSE huenda ikaathiriwa na mvua
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mitihani ya Kitaifa ya KCPE na KCSE huenda ikaathiriwa na mvua

Mitihani ya Kitaifa ya KCPE na KCSE huenda ikaathiriwa na mvua

Kuna hofu kuwa huenda mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Kilifi ikaathiri mitihani ya Kitaifa ya KCPE na KCSE. Inaarifiwa  madaraja yanayounganisha Shule ya Msingi na ya Upili ya Jimba yamefurisha kiasi kwamba hayapitiki.

Wanafunzi wamelazimika kusitisha masomo yao kwa muda kwa kukosa kufika shuleni kufuatia mvua hiyo.

Mwaka uliopita athari sawa na hiyo ilishughudiwa na kuwalazimu wanafunzi wa shule hizo kuhamishwa hadi shule nyingine jirani ili kufanya mitihani yao.

Kwenye Kaunti ya Kwale Shughuli za usafirika katika barabara kuu ya Likoni – Lungalunga zimetatizika baada ya daraja linalounganisha barabara hiyo katika eneo la Mamba kusomwa na mafuriko.

Naibu Kamishna wa Lunglunga Josphat Biwott amesema kwamba daraja hilo limeporomoka kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha .

Amesema kwamba tayari mipango ya kulikarabati daraja hilo inafanyika na wahanidisi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu KeNHA.

Kadhalika amewashauri madereva wanaohudumu kwenye barabara hiyo kutumia njia mbadala wakati daraja hilo linaendelea kurekebishwa.

Hayo yanajiri huku mvua hiyo kubwa ikitarajiwa kuendelea kunyesha kwenye  maeneo mbalimbali nchini.