array(0) { } Radio Maisha | Wakenya kupoteza mabilioni ya pesa kufuatia mradi wa vifaa vya afya.

Wakenya kupoteza mabilioni ya pesa kufuatia mradi wa vifaa vya afya.

Wakenya kupoteza mabilioni ya pesa kufuatia mradi wa vifaa vya afya.

Licha ya Wizara ya Afya kusisitiza kwamba serikali za kaunti hazistahili kulipia vifaa vya afya vilivyosambazwa kwa serikali hizo, imebainika kwamba huenda Wakenya wakapoteza  mabilioni ya pesa kufuatia mradi huo.

Stakabadhi zilizowailishwa kwa kamati maalum inayochunguza mradi huo zinaonesha kwamaba licha ya vifaa hivyo kutotumika Magavana wamelazimika kulipia jumla ya shilingi milioni mia mbili kila mwaka.

Waziri wa Afya Cisily Kariuki hata hivyo amepuuza madai kwamba magavana wanastahili kulipa kima cha shilingi bilioni 25 ili kunufaika na mradi huo, kauli iliyoibua mjadala mkali, huku maseneta wakimshtumu Kariuki kwa kutoa taarifa kinzani na ile aliyotoa awali.

Kariuki aidha alikuwa na wakati mgumu kujibu maswali kutoka kwa wanachama waliotakiwa kujua ni kwa nini baadhi ya vifaaa hivyo vimekuwa na hitilafu licha ya magavana kulipa ada za kila mwaka.

Ikumbukwe mwaka 2015 Wizara ya Afya ilitia saini mkataba na magavana kuhusu kusambaziwa kwa vifaa hivyo ambavyo vinegtolewa kwa hospitali mbili katika kila kaunti hatua ambayo wizara hiyo imezidi kusisitiza kwamba ililenga kuimarisha utoaji huduma katika kaunti.

Hata hivyo Magavana wameendelea kupinga mradi huo wakisema walishurutishwa kutia saini licha ya kutohusishwa kikamilifu katika mipango.