array(0) { } Radio Maisha | Idadi kubwa ya wakazi wa Ganda wajitokeza kushiriki uchaguzi mdogo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Idadi kubwa ya wakazi wa Ganda wajitokeza kushiriki uchaguzi mdogo

Idadi kubwa ya wakazi wa Ganda wajitokeza kushiriki uchaguzi mdogo

Idadi kubwa ya wakazi wa Ganda kwenye Kaunti ya Kilifi wamejitokeza kushiriki uchaguzi mdogo wa kumchagua mwakilishi wadi wao.

Licha ya mvua kubwa kunyesha na kudhaniwa kwamba ingetatiza shughuli hiyo, foleni ndefu za wapigakura zimeshuhudiwa katika vituo vya kura.

Jumla ya wapigakura elfu kumi na sita mia sita na thelathini wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo katika vituo thelathini vya kura.

Wagombea wanne akiwamo Reuben Katana wa Chama cha ODM, Mgombea huru Abdulrahiman Omar, Joseph Kiponda wa Jubilee na David Mitsanze wa Kadu Asili wanakiwania kiti hicho.

Afisa anayesimamia shughuli hiyo, Juma Musa amewaambia wanahabari kwamba shughuli yenyewe imeanza vyema na inaendelea bila changamoto zozote huku akieleza matumaini ya shughuli hiyo kukamilika mapema.

Aidha, Mkuu wa Polisi katika eneo la Kilifi Kaskazini - Patrick Njoroge amewahakikisha wakazi usalama wakati wa shughuli hiyo, akisema maafisa wa kutosha wa usalama wametumwa kudumisha amani.

Kwa upande wake Mbunge wa Kilifi Kaskazini, Owen Baya ambaye ametembelea Kituo Kikuu cha kuhesabia kura amekiri kuwapo kwa usalama huku wakazi wengi wakijitokeza kushiriki uchaguzi huo.