array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yamwachilia Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mahakama yamwachilia Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa

Mahakama yamwachilia Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa

Mahakama imemwachilia Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho ama shilingi laki tano pesa taslim.

Katika uamuzi wake, Hakimu Mkuu Vincent Adet amesema kiwango hicho cha dhamana pia kinamsimamia mshukiwa mwingine Geoffrey Oput Otieno aliyekamatwa pamoja na Jumwa.
 
Jumwa na Oput wameagizwa kujiwasilisha katika ofisi ya Mkuu wa Idara ya Upelelezi, DCI eneo la Malindi tarehe ishirini na mbili mwezi huu ili kusadia katika uchunguzi.
 
Adet aidha ameagiza upande wa mashtaka kutayarisha nyaraka za mashtaka dhidi ya Jumwa na Otieno na kuyawasilisha mahakamani mara moja.
 
Wakati uo huo, kundi la wanawake linalomuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto la Inua Mama, limeishtumu Idara ya Upelelzi DCI kwa kuwalenga wanasiasa wanaomuunga mkono Ruto. Muthoni Wamuchomba ni Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Kiambu.
 
Mwenzake wa Kirinyaga, Wangui Ngirichi amesema kukamatwa kwa Jumwa kunachochewa na baadhi ya maafisa walio na usawishi.
 
 
Aidha Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Uasin Gishu Gladys Shollei amesema watawasilisha malalamishi kwa Mamlaka ya Kuangazia Utendakazi wa Polisi IPOA kwa madai kuwa polisi walitumiwa vibaya kumzuilia Jumwa.
 
 
Jumwa alikamatwa Jumanne kufuatia virugu zilizoshuhudiwa  katika eneo la Mshongoleni, Wadi ya Ganda Kaunti ya Kilifi, na mauaji ya mtu mmoja.  Jumwa alidaiwa kuhusika pakubwa na maujai hayo madai ambayo hata hivyo aliyakana.