array(0) { } Radio Maisha | Eliud Kipchoge amerejea nchini

Eliud Kipchoge amerejea nchini

Eliud Kipchoge amerejea nchini

Mwanariadha Eliud Kipchoge amerejea nchini baada ya kuandikisha historia kwa kuvunja rekodi yake na kukimbia mbio ya kilomita 42 kwa saa moja, dakika 59 na sekunde arubaini.

Mkurugenzi wa mawasiliano katika Shirika la Kenya Airways, Dennis Kashero amesema Kipchoge aliwasili katika uwanja wa ndege wa JKIA saa kumi na mbili mapema leo, baada ya kusafiri kwa ndege ya KQ117 kutoka Amsterdam.

Kipchoge amerudi nchini humu siku tatu tu baada ya kuweka rekodi hiyo, jijini Viena kwa kaulimbiu ya no human is limited.

Hayo yakijiri Mshindi wa shindano la mbio za Chicago Marathon, upande wa wanawake Brigid Kosgei, pia amewasili nchini muda mchache uliopita.

Kosgei amepokelewa na Rais wa Shirikisho la Riadha Nchini, Jackson Tuwei ambaye amewapongeza wanariadha wa Kenya kwa kujizatiti katika kuiletea sifa nchi hii.

Wakati uo huo Tuwei amewashauri Wakenya kuwapigia-kura wanariadha walioteuliwa kuwania tuzo ya IAAF ya mwanariadha bora mwaka huu ili kuwahakikishia ushindi..