array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta amezindua Barabara ya JKIA - Westlands
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Rais Uhuru Kenyatta amezindua Barabara ya JKIA - Westlands

Rais Uhuru Kenyatta amezindua Barabara ya JKIA - Westlands

Rais Uhuru Kenyatta amewakashifu vikali watu wanaoukosoa ujenzi wa reli ya Kisasa huku akisisitiza umuhimu wa ujenzi wa reli hiyo kukamilika.

Akizungumza baada ya kuongoza uzinduzi wa Barabara ya JKIA - Westlands, Rais Kenyatta amesema uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa, SGR kati ya Nairobi na Suswa, niishara kwamba taifa hili linapiga hatua katika maendeleo.

Rais ametoa wito kwa Wakenya kushirikiana bila malumbano kuhusu miradi inayofanikishwa na serikali.

Katika kauli inayofikirika kurejelea vurugu zilizoshuhudiwa katika eneo la Ganda ambapo mtu mmoja ameuliwa na kusababisha mbunge wa Malindi Aisha Jumwa Kukamatwa, Rais Kenyatta amesisitiza haja ya Wakenya kujiepusha na siasa za uchochezi.

Ametumia firsa hiyo kukariri sababu iliyomfanya kupatana na Kinara wa ODM Raila Odinga huku akiwakashifu wanasiasa wanaopinga Handshake.

Wakati uo huo Rais ametetea mpango wa serikali kulenga kufanikisha ujenzi wa reli ya SGR kutoka Jijini Mombasa hadi Kisumu.

Amesema Kenya sawa na mataifa mengine, inalenga kuimarisha uchumi wa kitaifa kupitia mbinu za kisasa ukiwamo uchukuzi wa SGR.

Kuanzia kesho reli hiyo itaanza kuwasafirisha abiria katika vituo mbalimbalikati ya Nairobi na Suswa vikiwamo vituo vya Ngong Ongata Rongai na Nairobi Mjini.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, kutakuwa na safari za reli hiyo kati ya Ngong na Nairobi Ijumaa hadi Jumatatu.

Kisha kutakuwa na safari kati ya Nairobi na Suswa Jumapili pekee. Gharama ya usafiri kwa tikiti ya kawaida kati ya Nairobi na Ngong itakuwa shilingi 100, Ngong na Rongai shilingi 50, Rongai Suswa shilingi 100 na Nairobi Suswa shilingi 200. Itakuwapo safri kati ya Nairobi na Suswa Jumamosi.