array(0) { } Radio Maisha | Ruto apuuza taarifa kwamba Rais alikataa kuhudhuria kikao

Ruto apuuza taarifa kwamba Rais alikataa kuhudhuria kikao

Ruto apuuza taarifa kwamba Rais alikataa kuhudhuria kikao

Naibu wa Rais Dakta William Ruto amepuuza taarifa zilizochapishwa kwenye Gazeti moja la humu nchini zikidai kwamba njama yake ya kumshawishi Rais Uhuru Kenyatta kuhudhuria hafla moja ziliambuliwa patupu.

Gazeti hilo limechapisha kwamba Ruto alijaribu kumshawishi Rais Kenyatta kufanyaka kikao cha Wabunge wa Jubilee huku mpango wake ukiambulia patupu Juma lilopita huku Uhuru akielekea Bungeni kuwashawishi Wabunge kupitisha mapendekezo ya sheria ya ukopaji.

Ruto hajafurahishwa na taarifa hizo zilizochapishwa na Gazeti la Nation huku akiyataja kuwa bandia na kusisitiza kwamba yeye na Kenyatta ni kitu kimoja.


Ruto aidha amesema kwamba aliongoza kikoa cha Bajeti na Uchumi huku akipitsiha mapendekezo  kabla ya kikao cha wabunge  kufanyika.