array(0) { } Radio Maisha | Shughuli za kibiashara Taita Taveta, zathirika pakubwa

Shughuli za kibiashara Taita Taveta, zathirika pakubwa

Shughuli za kibiashara Taita Taveta, zathirika pakubwa

Shughuli za kibiashara maeneo mbalimbali kwenye kaunti ya Taita Taveta, zimeathirika pakubwa kufuatia kusombwa kwa barabara hasa sehemu za mashinani.

Wakizungumza na Radio Maisha wafanyabiashara hao wanasema hali hiyo imechangiwa na wanakandarasi waliopewa zabuni za kukarabati barabara hizo kukosa kuwajibika ikiwemo kutengeneza mitaro ya kuelekeza maji yanapostahili ili kuepuka hayo.

Katika Kaunti ya Mombasa, baadhi ya nyumba eneo la Tudor Moroto kwenye Kaunti ya Mombasa zimeporomoka kufuatia mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha kwenye Kaunti hiyo tangu jumamosi jioni siku mbili zilizopita.

Takwimu za Shirika la Msalaba Mwekundu Tawi la Mombasa zinazonesha kwamba mvua hiyo imesababisha kuta za jengo moja lilokuwa likijengwa eneo la Tudor karibu na Kanisa la Winners Chappel kuporomoka jana kufuatia mvua hiyo.

Baadhi ya maeneo ambayo yemekubwa na mafuriko ni Junda Mshomoroni, Kisauni, Bamburi, Kiembeni, Utange, Kadzandani, Kalahari, Bokole, Maweni na maneneo kadha ya Likoni.