array(0) { } Radio Maisha | Video ya dakika arubaini na saba iliyorekodiwa na Peter Ngugi haitachezwa

Video ya dakika arubaini na saba iliyorekodiwa na Peter Ngugi haitachezwa

Video ya dakika arubaini na saba iliyorekodiwa na Peter Ngugi haitachezwa

Video ya dakika arubaini na saba iliyorekodiwa na Peter Ngugi ambayo ilinuiwa kutumika kuwa ushahidi katika kesi ya mauaji ya wakili Willie Kimani haitchezwa mahakamani jinsi ilivyotarajiwa.

Hii ni baada ya Jaji Jessie Lessit kukubali ombi la Ngugi la kupinga kuchezeshwa kwa video hiyo. Katika video hiyo Ngugi aliwapeleka maafisa wa polisi maeneo yote ambayo alitembea na waliyoyafanya siku ambayo Wakili Kimani, Mteja wake na Dereva wa texi waliuliwa.

Jaji Lessit amesema Polisi ambaye alirekodi video hiyo hakuafuata sheria za wakati wa kunakili video hiyo kuwa ushahidi na kwamba haitachezeshwa mahakamani.

Mahakama aidha imeshangazwa na afisa anayeendesha uchunguzi wa mauaji ya Kimani Joseph Muindi kwa kuwa katika eneo la tukio wakati video iliporekodiwa.

Ikumbukwe wakili Kevin Michuki awali alipinga kuchezwa kwa video hiyo mahakamani akisema kuwa upande wa mashtaka haujafuata sheria zinazohusiana na namna ya ushahidi huo unavyopaswa kutumika, akiitaka mahakama kupinga hatua hiyo.