array(0) { } Radio Maisha | Mili ya Mariam Kighenda na mwanawe kufanyiwa upasuaji
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mili ya Mariam Kighenda na mwanawe kufanyiwa upasuaji

Mili ya Mariam Kighenda na mwanawe kufanyiwa upasuaji

Mili ya Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu walioaga dunia baada ya kuzama katika Kivuko cha Likoni wiki mbili zilizopita inatarajiwa kufanyiwa upasuaji Jumatatu. Mili hiyo imehifadhiwa katika Hifadhi ya Maiti ya Jocham tangu wiki iliyopita ilipoopolewa pamoja na gari walilozama nalo.

Kwa mujibu wa familia, kufikia sasa hawana tarehe rasmi ya mazishi ya wawili hao kwani hawajakabidhiwa mili rasmi na serikali ambayo imeweka kikwazio cha upasuaji huo kabla ya kuwakabadhi mili.

Familia hiyo imekuwa ikikutana katika eneo la Tudor Mombasa kwa ajili ya mipango ya mazishi huku jama, marafiki vilevile viongozi wakiendelea kuwatembelea kuwafariji wanafamilia hiyo.

Hayo yakijiri Mamlaka ya Usafiri wa Majini KMA kwa ushirikiano na idara nyingine za serikali imeanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho kilichoanzia kwa gari lililokuwa kwenye feri kutekeleza na kutumbukia majini kabla ya kuzama. Uchunguzi huo unatarajiwa kuangazia mikakati iliyowekwa kulinda usalama wa abiria.  Mmewe Kighenda, John Wambua amesema kwa sasa wanasubiri uchunguzi kuendelea ili kubaini kilichotokea.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kuhojiwa ni Meneja Mkurugenzi wa Shirika la Huduma za Feri Bakari Gowa na maafisa kadhaa wanaotarajiwa kufanya kazi chini yake.

Katika ujumbe wiki iliyopita, Rais Kenyatta aliapa kuhakikisha kwamba usalama wa safari za majini unaboreshwa