array(0) { } Radio Maisha | ODM na ANC sasa vinadai kuwepo kwa njama ya wizi wa kura Kibra
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

ODM na ANC sasa vinadai kuwepo kwa njama ya wizi wa kura Kibra

ODM na ANC sasa vinadai kuwepo kwa njama ya wizi wa kura Kibra

Vyama vya ODM na ANC sasa vinadai kuwepo kwa njama ya wizi wa kura katika uchaguzi mdogo wa tarehe 7 mwezi ujao wakati wa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kibra.

ANC ikiongozwa na Musalia Mudavadi ambaye aliandamana na mgombea wa wadhifa huyo kwa tiketi ya chama hicho Eliud Owalo amesema kwamba wamepokea taarifa ya kuwepo kwa mpango wa chama cha Jubilee kuwahonga wapingakura wakati wa uchaguzi huo ili kumwezesha mgombea wa chama hicho McDonald Mariga kuibuka mshindi.


Aidha, wabunge wa ODM ambao vilevile walikuwa eneo hilo kumpigia debe mgombea wao Imran Okoth walidai kwamba Naibu wa Rais William Ruto anatumia makazi yake rasmi kuendesha kampeni za kumpigia debe Mariga.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge wa Jubilee wameitaka Tume ya IEBC kukiondoa chama cha ODM katika Kinyanganyiro cha ubunge wa Kibra. Wabunge hao wakiwamo Kimani Ichungwa wa Kikuyu na Nixon Korir wa Lang'ata, wamemshtumu Mbunge wa Dagoreti Kaskasini Simba Arati kwa madai ya kulichochea kundi la vijana waliozua vurugu.

Wamesema wataiandikia  IEBC barua ya kuwasilisha malalamishi baada ya mabango ya Mariga kuharibiwa.  Hata hivyo chama cha ODM kimesisitiza kwamba hakikuhusika.

Ikumbukwe siku chache zilizopita Tume ya IEBC, ilisema inachunguza madai ya ODM kusema kuna njama ya watu fulani kufanikisha udanganyifu wakati wa Uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe saba mwezi ujao.

Ripoti ya uchunguzi huo inatarajiwa kutolewa juma hili.