array(0) { } Radio Maisha | Wakenya kugharamika zaidi kulipa madeni kupitia kodi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakenya kugharamika zaidi kulipa madeni kupitia kodi

Wakenya kugharamika zaidi kulipa madeni kupitia kodi

Hatma ya iwapo Wakenya watagharamika zaidi kwa kulipa madeni kupitia kodi, sasa i mikononi mwa wabunge.

Bunge la Kitaifa linatarajiwa kuuangusha au kuupitisha mswada wa kuifanyia marekebisha sheria za ukopaji wa madeni ili kuiwezesha serikali kukopa shilingi trilioni 3 zaidi.

Serikali inalenga kukopa shilingi bilioni 94. 2 kutoka African Development Bank, shilingi bilioni 6.9  za Uchina, bilioni 51 za World Bank na 30. 6 za AfD, bilioni 15. 9 kutoka Korea Kusini na bilioni 15. 3 za Ujerumani miongoni mwa mikopo kutoka kwa taasisi nyingine za kifedha.

Hatua hii inalenga kuiwezesha serikali kufanikisha ajenda nne kuu za serikali huku asimilia kubwa ikitarajiwa kutumika katika kuboresha huduma za afya. Majuma mawili yaliyopita Rais Kupitia Kaimu Waziri wa Fedha Ukur Yattani, aliwasilisha mswada bungeni wa kutaka marekebisho kufanywa kwenye sheria za ukopaji wa madeni ili kukopa shilingi trilioni 3 zaidi.

Ikumbukwe kwa sasa sheria hiyo inaizuia Kenya kukopa madeni zaidi ya mara tatu ikilinganishwa na pato la kitaifa GDP.

Hadi sasa deni la Kenya ni shilingi trilioni 5. 8 ikiwa ni asilimia 300 zaidi ya shilingi trilioni 1. 89 ambalo  Uhuru alirithi kutoka kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki mwaka 2013.