array(0) { } Radio Maisha | KUPPET yaunga mkono hatua ya TSC kusema itawaajiri maafisa wa nyanjani

KUPPET yaunga mkono hatua ya TSC kusema itawaajiri maafisa wa nyanjani

KUPPET yaunga mkono hatua ya TSC kusema itawaajiri maafisa wa nyanjani

Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri KUPPET kimeunga mkono hatua ya Tume ya Hudumza za Walimu TSC kusema itawaajiri maafisa wa nyanjani.

Mwenyekiti wa KUPPET Akello Misori amesema hatua hiyo itawapa fursa walimu waliohitimu kutoka vyuo mbbalimbali kupata tajrba.

Kauli yake imejiri baada ya Wizara ya Huduma za Umma kusema kwamba itawapa mafunzo nyanjani vijana mbalimbali waliohitimu kisha kuwaajiri katika idara mbalimbali za serikali katika kandarasi ya mwaka mmoja.

Kuhusu maslahi ya waliu, Misori amesema wanaendelea kusihinikiza serikali kuwapa marupurupu ya nyumba ya kati ya asilimia 30  na 70 ya mshahara wao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa KUPPET amesema watapinga mpango wa Wizara ya Elimu kuwatuma washauri kuhu masuala ya fedha katika shule za sekondari nchini.

Amewashauri walimu wanachama wake kuunga mkono mapendekezo ya chama kupigania haki zao