array(0) { } Radio Maisha | Kipchoge amevunja rekodi yake kwa kukimbia 42KM kwa 1::59:40
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kipchoge amevunja rekodi yake kwa kukimbia 42KM kwa 1::59:40

Kipchoge amevunja rekodi yake kwa kukimbia 42KM kwa 1::59:40

Mwanariadha Eliud Kipchoge amevunja rekodi yake mwenyewe na kuandikisha historia kwa kuwa mwanadamu wa kwanza kukimbia Marathon ya Kilomita arubaini na mbili kwa kutumia muda wa saa moja dakika hamsini na tisa na sekunde arubaini.

Mwanariadha huyo ameelezea furaha  baada ya kumaliza mbio hizo.

Kipchoge amesema lengo Kuu lake ni kuhakikisha kuwa riadha inatambulika kuwa safi, huku akitoa shukrani kwa wote waliochangia kufanikiwa wake.

 ''Nimejaribu, mimi ndiye mwanadamu wa kwanza kukimbia chini ya saa mbili, nataka kuwapa watu wengi motisha, niwaeleze kuwa hakuna mwanadamu asiyeweza lolote''

''Wasaidizi wangu 41 ni miongoni mwa wanariadha bora duniani kote, wawashukuru kwa kukubali kuifanya kazi hii''

''Spoti ni muhimu nataka kuifanya riadha kuwa spoti safi'' Kipchoge        

Wakati uo huo, Mkewe Eliud Kipchoge, Grace amesema kuwa anafurahia kushuhudia Mumewe akijaribu kukimbia chini ya saa mbili.

Kocha wake Partrick Sang' amesema Kipchoge alijitolea zaidi na kwamba ameliweka taifa hili.

''Nimefurahi sana kwa mafanikio yake. Kwa kweli ametupa motisha sisi sote    kwamba tunaweza kufanya chochote zaidi ya uwezo wetu jinsi tunavyodhani'' Sang'

Mbio hizi zilithaminiwa na Sir Jim Arthur Ratcliffe ambaye pia ndiye muasisi wa tukio hili ambalo limeisisimua dunia mzima kwa sasa. Ratcliffe ni  mtaalamu wa uhandisi wa kemikali na mmiliki wa kampuni ya Ineos Chemical. Kampuni hiyo hupata shilingi trilioni 9 kila mwaka.  Ratcliffe amesema kwamba lengo lake pamoja na Kipchoge vile vile timu nzima iliyojitolea limetimia.

Kipochoge alilenga kutumia muda wa saa moja dakika hamsini na tisa.

Mbio za INEOS1;59 ni za aina yake na hata kama hazitatambuliwi na Shirikisho la Riadha Duniani IAAF,  Kipchoge amethibitisha kuwa ana uwezo baada ya kuwa mwanadamu wa kwanza kukimbia chini ya saa mbili. 

Ikumbukwe kuwa Kipchoge alikosa sekunde ishirini na sita jijini Monza Italia akijaribu kuvunja rekodi ya kukimbia chini ya saa mbili, mwaka 2017.

Je, wajua kwamba mara ya mwisho binadamu kuandikisha histroia katika spoti ilikuwa  miaka sitini na mitanop iliyopita Kipchoge amefanikiwa kuandikisha historia hiyo baada ya  Roger Bannister raia wa Uingereza.