array(0) { } Radio Maisha | Fatuma Gedi awaongoza viongozi wa Odm kumpigia debe Imran

Fatuma Gedi awaongoza viongozi wa Odm kumpigia debe Imran

Fatuma Gedi awaongoza viongozi wa Odm kumpigia debe Imran

Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Wajir, Fatuma Gedi amewaongoza viongozi wengine wa eneo la Kaskazini kumpigia debe mgombea wadhifa wa ubunge eneo la Kibra kwa tiketi ya Chama cha ODM, Imran Okoth.

Gedi ameendeleza shutma dhidi ya Chama cha Jubilee kwa kumteua MacDonald Mariga kupeperusha bendera ya chama hicho. Gedi amesema Jubilee ilipotoka kwa kukosa kuandaa shughuli ya utezi kabla ya kumchagua Mariga.

Imran amendamana na Gedi, Mbunge wa Wajir Kaskazini Ahmed Ibrahim, Abdikarim Osman wa Fafi, Seneta Abshiro Halake na Anthony Oluoch wa Mathare, ambao kwa pamoja wametoa wito kwa wakazi wa Kibra kumuunga mkono Okoth, wakisema ana uwezo wa kuafikia mabadiliko kwa kuwa anafahamu vyema masaibu ambayo wanapitia.

Jumatano viongozi wa ODM walifanya mkutano na viongozi wa Tume ya Uchaguzi IEBC kuhusu shinikizo la kutaka kupewa sajili ya wapiga-kura.