array(0) { } Radio Maisha | Shughuli ya kuliopoa gari lililozama Likoni inaendelea

Shughuli ya kuliopoa gari lililozama Likoni inaendelea

Shughuli ya kuliopoa gari lililozama Likoni inaendelea

Shughuli ya kuliopoa gari lililozama katika Kivuko cha Likoni baada ya kudondoka kutoka ndani ya feri inaendelea. Kwa sasa kreni inalivuta gari hilo na muda mfupi kutoka sasa litakuwa nje ya maji.

Shughuli hiyo inafanywa na maafisa wa Jeshi la Wanamaji, wale wa Halmashauri ya Bandari, maafisa wa Kenya Feri na wapiga-mbizi kutoka Afrika Kusini. Maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu wako tayari na mifuko ya kubebea maiti.

Aidha, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji Levy Mghalu, Gavana wa Mombasa Hassan Joho pamoja na viongozi wa kidini wako eneo hilo huku Msemaji wa Serikali, Cyris Oguna akitarajiwa kuwahutubia wanahabari kwa mara ya mwisho kuhusu uopozi huo.

Licha ya mvua inayoendelea kunyesha kwenye Kaunti ya Mombasa, dalili zipo kwamba shughuli hiyo itakamilika leo.