array(0) { } Radio Maisha | Abiria hamsini na watano akiwamo rubani wamenusurika kifo

Abiria hamsini na watano akiwamo rubani wamenusurika kifo

Abiria hamsini na watano akiwamo rubani wamenusurika kifo

Abiria hamsini na watano akiwamo rubani wamenusurika kifo mapema Ijumaa baada ya ndege waliyokuwa wameabiri kuanguka. Ndege hiyo ya Kampuni ya Silverstone ilianguka dakika chache tu baada ya kupaa katika Uwanja wa Ndege wa Wilson.

Wakati uo uo, Idara ya Upelelezi DCI imesema inachunguza ajali hiyo.

Katika taarifa kwa vyombo vya Habari Mamlaka ya Usalama wa Viwanja vya Ndege, KAA aidha imesema miongoni mwa abiria hao wawili walipata majeraha madogo na wanaendelea kutibiwa.

Awali, Kampuni ya Silverstone ilisema abiria wote hamsini waliokuwa katika ndege iliyoanguka katika Uwanja wa Wilson waliondolewa, huku ukiahidi kushirikiana na idara zinazohusika ili kubaini kilichoababisha ndege hiyo kuanguka muda mfupi tu baada ya kutwaa.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu liliripoti kuwa huenda ndege hiyo ilikumbwa na hitilafu za mitambo.

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Lamu.