array(0) { } Radio Maisha | Kipchoge atavunja rekodi yake ya saa mbili katika mbio za INEOS 159

Kipchoge atavunja rekodi yake ya saa mbili katika mbio za INEOS 159

Kipchoge atavunja rekodi yake ya saa mbili katika mbio za INEOS 159

Wizara ya Michezo nchini imeeleza matumaini kuwa bingwa wa mbio za marathon, Eliud Kipchoge kwamba atavunja rekodi yake ya saa mbili katika mbio za INEOS jijini Viena Austria.

Wakati wa kikao na wananahabari mapema leo, Waziri wa Michezo Balozi Amina Mohamed amesema mazoezi ambayo Kipchoge amekuwa akishiriki yanatosha kumwezesha kuivunja rekodi yake ya saa moja dakika hamsini na tisa.

Amina aidha amewashauri wananchi kujitokeza kwa wingi katika Jumba la Mikutano la KICC kushuhudia Kipchoge akishiriki mbio hizo. Amesema Wizara ya Michezo itaweka televisheni kubwa katika jumba hilo ili kuwaruhusu wananchi walio karibu kumfuatilia mbio yenyewe.

Kipichoge ambaye ndiye bingwa wa Olympiki katika marathon aliwasili jijini Viena Jumanne wiki hii. Akizungumza na wananahabari baada ya kuwasili Kipchoge alieleza matumaini ya kufanya vizuri zaidi.