array(0) { } Radio Maisha | Kulikoni Likoni?
Kulikoni Likoni

Na Caren Papai

NAIROBI, KENYA, Huku shughuli ya kuliondoa gari lililozama katika Kivuko cha Likoni likiwa na Mariam Kigenda na Mwanawe Amanda Mutheu ikiendelea, shughuli nzima ya uopoaji imesemekana kuathiri pakubwa safari za meli nje na ndani ya Bandari ya Mombasa kuanzia Septembe 29 ambapo wawili hao walizama.

Takribani meli sita zinaendelea kusubiri kukamilika kwa shughuli hiyo kabla ya kuondoka kwenye bandari hiyo.

Msemaji wa serikali Kanali Mstaafu, Cyrus Oguna amesema shughuli hiyo iliyotarajiwa kuchukua muda wa saa tatu huenda ikauchukua muda zaidi kuliko ilivyotarajiwa kufuatia mawimbi makali baharini.

Oparesheni ya kuliondoa gari hilo lililo mita hamsini na nane ndani ya bahari katika Kivuko cha Likoni inaendelezwa na vitengo mbalimbali vya shughuli hiyo likiwamo Jeshi la Wanamaji.

Meli maalum yenye kreni iko eneo lililo gari hilo huku uchukuzi kwenye kivuko hicho ukiendelea kando badala ya katikati ya kivuko ambapo oparesheni hiyo inaendelea.