array(0) { } Radio Maisha | Ngugi Thiong'o miongoni mwa wanaowania tuzo ya Nobel

Ngugi Thiong'o miongoni mwa wanaowania tuzo ya Nobel

Ngugi Thiong'o miongoni mwa wanaowania tuzo ya Nobel

Na Caren Omae,

NAIROBi, KENYA, Mwandishi maarufu kutoka nchini Kenya, Prof Ngugi wa Thiong'o ni miongoni mwa waandhisi kadhaa wanaosubiri kubaini iwapo watatwaa tuzo ya Nobel katika uandhisi mwaka huu.

Tuzo hiyo itatolewa kwa watu wawili baada ya kuahirishwa mwaka uliopita kufuatia sakata iliyochipuza katika bodi ya uteuzi.

Mbali na Ngugi wa Thiong'o wengine waliotajwa kuwa na nafasi bora ya kutuzwa ni Lyudmila Ulitskaya wa Urusi, Olga Tokarzguk wa Poland, Can Xue wa Uchina na Maryse Conde. Wengine ni waandishi kutoka Canada, Mar Atwood na Anne Carson.

Mshindi atakabidhiwa shilingi milioni 93, medali na stashahada yaani Diploma.