array(0) { } Radio Maisha | Hisia kinzani zatolewa kuhusu kutimuliwa kwa Samboja
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Hisia kinzani zatolewa kuhusu kutimuliwa kwa Samboja

Hisia kinzani zatolewa kuhusu kutimuliwa kwa Samboja

Na Sam Amani,

NAIROBI, KENYA, Hisia mbalimbali zinaendelea kuibuka miongoni mwa wakazi wa Kaunti ya Taita Taveta baada ya wawakilishi wa wadi katika kaunti hiyo kupiga kura kumuondoa mamlakani Gavana Granton Samboja.

Baadhi ya wakazi waliozungumza na wanahabari wamemlaumu Samboja kwa kuchelewesha mchakato wa kuivunja serikali yake licha ya kuanza kukusanya saini zilizolenga kufanikisha hatua hiyo. Kulingana nao wadi ishirini tayari zimeshirikishwa huku takribani saini elfu hamsini na mbili zikisainiwa kwa ajili ya kulivunja bunge hilo.

Kwa upande mwingine, wakazi wamemlaumu Samboja kwa madai ya kuzembea kazini huku huduma muhimu zikikosa kufanikishwa mashinani. Wameunga mkono hatua ya kutimuliwa mamlakani

Aidha katika mazungumzo ya awali yaliyowahusisha viongozi wa dini mbalimbali, Wafanyabiashara, Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa, Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga na Naibu wa Rais William Ruto, Samboja alishauriwa kukumbatia mazungumzo kati yake na Wawakilishi wa Wadi katika kaunti hiyo.

Wawakilishi wadi katika kaunti hiyo wamesema wamekuwa wakishinikiza kuwapoa kwa mazungumzo ili kusitisha mzozo unaoikumba serikali hiyo ila gavana Samboja amekuwa akilemaza juhudi zao, Meshack Maghangha ni spika wa kaunti hiyo.