array(0) { } Radio Maisha | Gari linaloaminika kuwa lile lilolozama likiwa na mama na mwanawe katika Kivuko cha Likoni limepatikana

Gari linaloaminika kuwa lile lilolozama likiwa na mama na mwanawe katika Kivuko cha Likoni limepatikana

Gari linaloaminika kuwa lile lilolozama likiwa na mama na mwanawe katika Kivuko cha Likoni limepatikana

 

Gari linaloaminika kuwa lile lililozama na Mariam Kigenda na mwanawe Amanda Mutheu linatarajiwa kuondolewa baharini baada ya kutambulika liliko.

Msemaji wa Serikali Kanali Mstaafu Cyrus Oguna amesema mtambo wenye kamera maalumu umetumika kubaini kifaa kinachoaminika kuwa gari hilo majini.

Amesema Jeshi la Wanamaji litashirikiana na wapigambizi wengine kuliopoa gari hilo.

Hata hivyo Oguna amesema kwa sasa hawezi kuthibitisha iwapo mili ya Mariam na mwanawe ingali ndani ya gari hilo, baada ya kukaa majini kwa takribani siku kumi na moja zilizopita.

Oguna amesema gari hilo ambalo limeonekana kupitia mitambo ya kisasa ya kamera za 3HD liko mita hamsini na nane ndani ya bahari.

Amesema kwa sasa uchunguzi unaendelea ili kuthibitisha nambari za usajili wa gari hilo.

Oguna amesema imesalia asilimia kumi pekee ya shughuli hiuo ili kufaulisha uopoaji wa mili ya waliozama.

Amelipongeza Jeshi la Wanamaji na wapingambizi wanaoendesha shughuli hiyo.

Msemaji wa familia ya waliozama Luke Mbati alikataa kuzungumza na wanahabari kwa kushikilia kwamba atazungumza baada ya mili hiyo kuopolewa.

Kigenda na mwanawe walizama baharini tarehe 29 mwezi uliopita baada ya gari lao kuteleza kutoka kwenye Feri ya MV Harambee kwenye Kivuko cha Likoni.