array(0) { } Radio Maisha | IEBC kuchunguza madai ya udanganyifu wakati wa uchaguzi mdogo, Kibra
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

IEBC kuchunguza madai ya udanganyifu wakati wa uchaguzi mdogo, Kibra

IEBC kuchunguza madai ya udanganyifu wakati wa uchaguzi mdogo, Kibra

Tume ya Uchaguzi IEBC imekubali kukipa Chama cha ODM sajili ya wapigakura inayotumika katika shughui ya uchaguzi mdogo utafkaofanyika Noveba tarehe 7 ili kuitathimini kubaini iwapo haina dosari. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema wapigakura wote waliosajiliwa kwenye eneo bunge hilo watauhusiwa kupigakura.

Aidha amewataka wote waliojisajili kuanzia mwaka jana, kuhakikisha kuwa majina yao yanajumuishwa katika sajili itakayotumika ambayo itakamilika wiki ijayo.

Wakati uo huo, Chebukati amesema watawatuma maafisa wake kufanya uchunguzi kuhusu madai njama ya kutekeleza udanganyifu wakati wa uchaguzi huo ili kubaini ukweli.

Mwenyekiti wa Chama cha ODM John Mbadi kwa upande wake amesema wameshauriana na IEBC majina ya wapigakura waliosajiliwa Kibra baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 yatajumuishwa katika sajili itakayotumika wakati wa uchaguzi huo mdogo.