array(0) { } Radio Maisha | Nembo mpya ya M-Pesa kwa siku 7 zijazo #Eliud159

Nembo mpya ya M-Pesa kwa siku 7 zijazo #Eliud159

Nembo mpya ya M-Pesa kwa siku 7 zijazo #Eliud159

Kampuni ya Safaricom imezindua nembo ya M-pesa itakayotumika kwa siku saba zijazo kwa heshima ya mwanariadha Eliud Kipchoge.

Nembo hiyo mpya itakuwa na maneno matano ya jina la Kipchoge, ELIUD na nambari 1:59 muda ambao Kipchoge anatarajiwa kuutumia kukimbia Jumamosi hii jijini Vienna, Austria.

Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Safaricomn Micheal Joseph amesema hatua hiyo ni ya kumenzi Kipchoge kuwa mwanariadha aliye na kipaji vile vile kwa kuliweka taifa hili mbele kwenye riadha.

Kipchoge aliyewasili Vienna Jumanne anaendelea na matayarisho yake kabla ya Jumamosi.