array(0) { } Radio Maisha | ODM kuandamana Jumatano dhidi ya IEBC
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

ODM kuandamana Jumatano dhidi ya IEBC

ODM kuandamana Jumatano dhidi ya IEBC

Joto la siasa za uchaguzi mdogo wa Kibra linatarajiwa kupanda leo huku Chama cha ODM kikitarajiwa kurejelea maandamano dhidi ya IEBC kikilalamikia njama ya kuhitafiana na uchaguzi Kibra. 

Kupitia kikao na wanahabari, chama hicho kimsema kuwa kitafanya maandamano katika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi IEBC kuishinikiza kutoa orodha ya wapigakura watakaoshiriki uchaguzi mdogo wa Kibra.

Akiwahutubia wanahabari katika majengo ya bunge, Mwenyekiti wa ODM John Mbadi, ameikashifu IEBC kwa madai ya kuwa na njama ya kufaulisha wizi wa kura, wakati wa uchaguzi mdogo Novemba 7 mwaka huu kwa kukataa kuweka wazi sajili ya wapiga kura itakayotumika wakati wa shughuli hiyo.

Kwa  mujibu wa Mkuu wa Uchaguzi chamani Junet Mohamed  waliandika barua zaidi ya mara tatu kupitia katibu mkuu vilevile kamouni za mawakili kabla ya barua yao kujibiwa na Afisa Mkuu Mtendaji Marjan Hussein ambaye aliwataka kulipa shilingi elfu 15, fedha ambazo zililipwa mara moja.

Kwa mujibu wa Junet, IEBC imekataa kuwapa sajili hiyo na hivyo kutia nguvu madai ya mikutano ya kisiri na njama ya kuhitilafiana na shhughuli hiyo iliyorataibiwa Novemba tarehe 7. Junet amemtaja aliyekuwa Waziri wa Kawi Davis Chirchir kuwa miongoni mwa wanaohusishwa katika njama hiyo.

Hata hivyo katika taarifa ya hivi punde zaidi, IEBC imesema kwamba sajili hiyo sasa iko  katika harakati za kuchunguzwa katika ofisi ya Afisa Mkuu wa  Uchaguzi wa Kibra kwa siku saba kabla ya sajili ya mwisho kusambazwa kwa wote wanaoihitaji. Hata hivyo, suala kuu ni iwapo chama cha ODM kilifahamishwa kuhusu utaratibu huu  au la  kwani chama cha ODM kinalalamikia kimya cha IEBC katika mawasiliano ya kusaka  sajili hiyo.