array(0) { } Radio Maisha | M-Pesa imetajwa kuwa miongoni mwa mifumo 10 ya kibiashara inayokuza uchumi

M-Pesa imetajwa kuwa miongoni mwa mifumo 10 ya kibiashara inayokuza uchumi

M-Pesa imetajwa kuwa miongoni mwa mifumo 10 ya kibiashara inayokuza uchumi

Mfumo wa kutuma na kupokea fedha kwa simu M-pesa umetajwa kusaidia pakubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.

Mpesa inayomilikiwa na Kampuni ya Mawasiliano Safaricom, imeorodheshwa na Taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo PMI kuwa miongoni mwa mifumo kumi ya kibiashara, iliyochangia kwenye ukuaji wa kiuchumi katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita

Zaidi ya mifumo elfu moja ya kibiashara ilihusishwa kwenye utafiri huo, ambapo M-Pesa imeibuka kuwa miongoni mwa bora zaidi.