array(0) { } Radio Maisha | Mudavadi amkashifu vikali Naibu wa Rais William Ruto

Mudavadi amkashifu vikali Naibu wa Rais William Ruto

Mudavadi amkashifu vikali Naibu wa Rais William Ruto

Kiongozi wa Chama cha Amani National Congress, ANC Musalia Mudavadi amekashifu hatua ta Naibu wa Rais William Ruto kutumia makazi yake rasmi eneo la Karen kuendesha mikutano ya kisiasa.

Akihutubu wakati wa mkutano na wafuasi wa ANC jijini Nairobi, Mudavadi ambaye amekuwa ziarani ughaibuni, amesema inasikitisha kwamba Ruto anatumia mali ya umma kuendesha kampeni za mwaka 2022 pamoja na uchaguzi mdogo wa tarehe 7 mwezi ujao wa eneo la Kibra.

Ikumbukwe kuwa ANC itashiriki uchaguzi huo mdogo huku mgombea wake akiwa Eliud Owalo.