array(0) { } Radio Maisha | Mombasa: Waganga wapendekeza kujengewa ofisi katika hospitali za umma

Mombasa: Waganga wapendekeza kujengewa ofisi katika hospitali za umma

Mombasa: Waganga wapendekeza kujengewa ofisi katika hospitali za umma

Baadhi ya waganga wa kienyeji kwenye Kaunti ya Kwale wanapendekeza kujengewa ofisi katika hospitali za umma ili kusaidia  kuwatibu wagonjwa ambao maradhi yao yamewatataiza madaktari hospitalini.

Mwenyekiti wa Waganga kwenye Kaunti hiyo Mwakusema Hamisi Makweli amesema hali hiyo itawapunguzia gharama baadhi ya wagonjwa ambao hulazimika kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu.

Kuhusu kukithiri kwa visa vya wazee kutengwa na jamii kwa kushukiwa kuwa wachawi, Makweli amesema baadhi ya waganga wamekuwa wakichangia katika suala la kuwaharibia wenzeo sifa kufuatia ushindani.