array(0) { } Radio Maisha | Usalama katika kivuko cha Likoni waendelea kutiliwa shaka

Usalama katika kivuko cha Likoni waendelea kutiliwa shaka

Usalama katika kivuko cha Likoni waendelea kutiliwa shaka

Suala la usalama kwa wanaotumia Kivuko cha Likoni linaendelea kuibua hisia mseto miongoni mwa viongozi wa kisiasa katika Kaunti ya Mombasa.

Mbunge wa Jomvu, Badi Twalib amekuwa wa hivi punde kueleza masikitiko yake kuhusu jinsi ambavyo Shirika la Huduma za Feri halijaweka mikakati ya kukabili majanga yanapotokea.

Kulingana naye, shirika hilo limezembea katika utendakazi wake huku akishinikiza liwajibikie mkasa wa kuzama kwa Mariam Kighenda na mwanamwe, Amanda Mutheu.

Hayo yanajiri huku vikosi vya wapiga-mbizi zinavyowajumuisha wapiga-mbizi kutoka Afrika Kusini wa Kampuni za Sub-sea na Southern Engineering vikiendelea kuyakagua maeneo manne ambayo yanakisiwa gari lililozama na mili ya wawili hao lilikwama.

Oparesheni ya kuitafuta mili ya Mariam na mwanamwe kwa siku ya tisa sasa haijazaa matunda huku familia ya marehemu ikiendelea kukita kambi kandokando ya kivuko hicho huku wakiendeleza ibada za kuiombea oparesheni hiyo ifaulu.