array(0) { } Radio Maisha | Spika Muturi akashif Marekani kwa kukataa kutangaza Kundi la Alshabaab kuwa la kigaidi

Spika Muturi akashif Marekani kwa kukataa kutangaza Kundi la Alshabaab kuwa la kigaidi

Spika Muturi akashif Marekani kwa kukataa kutangaza Kundi la Alshabaab kuwa la kigaidi

Spika wa Bunge la Kitaifa Justine Muturi, amelilamu vikali taifa la Marekani kwa kukataa ombi la Kenya kushinikiza Kundi  la Alshabaab kutangazwa na taifa hilo kuwa la kigaidi.

Muturi amesema hatua ya Marekani kukataa kulitangaza kundi hilo kuwa la kigaidi inaendelea kutoa mwanya kwa Alshabaab kupokea ufadhili kutoka kwa mataifa ya kigeni ,hivyo basi kuwapa wanachama wake nguvu ya kuendelea kutatiza amani katika mataifa mbalimbali likiwamo Kenya.

Spika Muturi amedai kwamba kundi hilo kutoka Somali linaendela kupata kinga kutoka mataifa yaliyostawi kupitia mashirika ya kijamii yanayojifanya kuwa yakutetea haki za binadamu. Muturi adha ameonya kwamba hatua hiyo imesambaratisha juhudi ambazo zimewekwa na Kenya kukabali makundi ya kigaidi.

Hata hivyo, Balozi wa Marekani humu nchini Kyle McCarter amepinga kauli ya Muturi ,akisema taifa la Marekani linaunga mkono Azimio la 751 la Umoja wa Mataifa kutangaza Alshabaab kuwa kundi la kigadi.

Mac Carter amesema taifa lake linaendeleza juhudi za kulikabili kundi hilo huku akisema Marekani haiwezi kukubali ombi la Kenya kukatiza misaada ya kibinadamu kwa Somalia. Viongozi hao wamekuwa wakizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la Usalama wa Bunge mapema leo hii.

Muturi amesema kongamano hilo litatoa fursa ya wabunge kubuni mikakati ya kukabili ugaidi kupitia utungaji wa sheria bungeni.