array(0) { } Radio Maisha | Kesi ya mauaji ya wakili Willie Kimani yachukua mkondo mpya

Kesi ya mauaji ya wakili Willie Kimani yachukua mkondo mpya

Kesi ya mauaji ya wakili Willie Kimani yachukua mkondo mpya

Vikao vya kusikiliza kesi ya mauji ya wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na dereva wa texi Joseph Muiruri ,vimefanyika siku ya Jumatatu mahakamani huku maelezo ya kutisha kuhusu maujia hayo yakitolewa.

Afisa wa polisi Peter Ngugi kupitia Afisa wa Idara ya Upelelezi DCI  Geofrey Kinyua,  ameelezea mahakama jinsi watatu hao walivyofuatiliwa, kunaswa, kuteswa na kisha kuuliwa na miili yao kutupwa ndani ya Mto Athi, karibu na Kituo cha Polisi cha Donyo Sabuk.

Shahidi huyo alisema kwamba walianza kuwafuatwa watatu hao baada ya Sergenti  Fredeick Ole Leliman kuwaarifu kuhusu njama ya kumuua Joseph Mwenda muhudumu wa bodaboda ,ambaye alikuwa amewasilisha kesi mahakamani dhidi yake.

Afisa huyo aidha ameiambia mahakama kwamba walimfuata Mwenda katika Mahakama ya Mavoko ,ambapo kesi hiyo ilichukuwa muda wa saa mbili kabla yao kuwateka nyara.

Amesema kazi yake ilikuwa kuiondoa miili ya watatu hao kutoka nyuma ya gari baada ya kuuliwa.  Ngugi aidha ameeleza jinsi Mwenda alikuwa wa kwanza kuuliwa mwendo ya saa nne usiku kwa kunyongwa kutumia kamba,  Muiruri na kisha Kimani.

Maafisa wanne wa polisi Fredrick Leliman, Stephen Cheburet, Sylvia Wanjiku, Leonard Mwangi pamoja na Ngugi wamehusishwa na mauaji hayo ya Juni 23 mwaka wa 2016.