array(0) { } Radio Maisha | Eneo la Oparesheni za Kijeshi katika Kivuko cha Likoni lafungwa kwa muda

Eneo la Oparesheni za Kijeshi katika Kivuko cha Likoni lafungwa kwa muda

Eneo la Oparesheni za Kijeshi katika Kivuko cha Likoni lafungwa kwa muda

Eneo la Oparesheni za Kijeshi katika Kivuko cha Likoni limefungwa kwa muda ili kutoa nafasi kwa Jeshi la Wanamaji na wapiga-mbizi wa Afrika Kusini kuendeleza shughuli ya kuiopoa mili ya Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu waliozama wiki iliyopita.

Maafisa wa Jeshi la Wanamaji, Kenya Navy wakishirikiana na wapiga-mbizi hao, wanaendesha shughuli hiyo kwa siku ya nane sasa huku serikali ikitumia vifaa maalum vyenye uwezo wa kupiga picha kwa mbali, ili kuwawezesha kukamilisha shughuli hiyo kwa wakati.

Mwenyekiti wa Shirika la Huduma za Feri, Dan Mwazo amesema tayari wapiga-mbizi waliojukumiwa na familia ya Mariam kuiopoa mili hiyo wameingia majini kushirikiana na wale ambao wameletwa na serikali. Amesema kikosi hicho kinatarajiwa kupata vifaa vingine ambavyo vitatumika kesho, iwapo hawatafanikiwa kuipata mili hiyo hii leo.