array(0) { } Radio Maisha | uopoaji wa miili eneo la Likoni wasitishwa

uopoaji wa miili eneo la Likoni wasitishwa

uopoaji wa miili eneo la Likoni wasitishwa

Shughuli za uopoaji wa miili ya mama na mwanawe waliotumbukia ndani ya Bahari Hindi imesitishwa kwa muda.

Wakuu wa Shirika la Huduma za Feri wamesema kwamba shughuli hiyo imesitishwa muda mfupi uliopita ili kutoa fursa kwa meli kutoka India kutua katika Bandari ya Mombasa.

Taarifa hii inajiri wakati ambapo serikali ikiwa tayari imedokeza kwamba itawashirikisha wataalam kutoka Afrika Kusini kusaidia katika shughuli hiyo ya uopoaji. Vilevile, Msemaji wa Serikali Kanali Cyrus Oguna ametangaza kwamba watatumia mashine maalum kutambua liliko gari hilo lililoanguka kutoka kwa Feri wiki moja iliyopita.