array(0) { } Radio Maisha | Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia ajali

Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia ajali

Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia ajali

Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia ajali ya Barabarani kwenye eneo la Gilgil, Nakuru.


Ajali hiyo imetokea baada ya malori mawili kugongana ana kwa ana. Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Nkauru Stephen Matu amesema ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa lori moja lililokuwa likielelea Nairobi kujaribu kulipita gari jingine na kuligonga lori lililokuwa likitokea upande wa pili.


Waliojeruhiwa wnaendelea kutibiwa katika hospitali ya St. Mary's, huku mili ya waliofariki dunia ikipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Gilgil