array(0) { } Radio Maisha | PSC kuzindua mpango wa kuwapa mafunzo wanafunzi Nairobi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

PSC kuzindua mpango wa kuwapa mafunzo wanafunzi Nairobi

PSC kuzindua mpango wa kuwapa mafunzo wanafunzi Nairobi

Kamati ya Huduma za Umma, PSC inatarajiwa kuzindua mpango wa kuwapa mafunzo wanafunzi wanaotumwa nyanjani, Interns Jumatano wiki hii hapa jijini Nairobi.

Waziri wa Huduma za Vijana na Masuala ya Jinsia, Profesa Margaret Kobia na Mwenyekiti wa PSC, Stephen Kirogo pamoja na wakuu wengine serikalini na sekta ya binafsi wameratibiwa kuzindua rasmi mafunzo hayo.

Tayari kamati hiyo imewatumia ujumbe wanafunzi hao 3,100 ili kuhudhuria mafunzo hayo ya siku mbili mnamo Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

Walioteuliwa ni miongoni mwa wanafunzi elfu kumi na nane waliotuma maombi katika kaunti zote arubaini na saba.

Wanafunzi hao wa nyanjani watatumwa katika wizara mbalimbali, idara za serikali vilevile taasisi mbalimbali nchini ambapo watahudumu kwa mwaka mmoja huku wakilipwa kiwango fulani cha fedha kila mwezi.

Wanatarajiwa kuhudumu chini uangalizi wa maafisa waliohitimu na wenye tajriba ili kupata ujuzi wa kuwawezesha kupata kazi katika siku za usoni.

Ikumbukwe bunge lilitenga shilingi bilioni moja kugharimia mpango huo katika mwaka wa kifedha 2019/2020.