array(0) { } Radio Maisha | Alfred Mutua awata viongozi wa kini kutoa mwelekeo nchini

Alfred Mutua awata viongozi wa kini kutoa mwelekeo nchini

Alfred Mutua awata viongozi wa kini kutoa mwelekeo nchini

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amesema viongozi wa kidini wana jukumu kubwa la kutoa mwelekeo kwa wakenya katika juhudi za kukabili ufisadi nchini. Katika taarifa kwa vyombo vya habari leo hii, Mutua ametoa changamoto kwa viongozi hao kuendelea  kukataa michango ya kifedha ambayo inakisiwa kutolewa na viongozi fisadi.

Gavana Mutua aidha amesema kuna haja ya kuwahamasisha wakristo kuhusu kuwachagua ambao hawajahusishwa na sakata na hasa wanaohusishwa na masuala ya kuwakandamiza wananchi.

Kauli hii inajiri siku moja baada ya Maaskofu wa kanisa la Katoliki kutoa mwelekeo mpya katika makanisa yao kote nchini  kuhusu swala la kupokea  michango au ufadhili wa kifedha kutoka kwa viongozi wa kisiasa.