array(0) { } Radio Maisha | Mbarak awapongeza maaskofu wa katoliki kwa kupiga marufuku michango

Mbarak awapongeza maaskofu wa katoliki kwa kupiga marufuku michango

Mbarak awapongeza maaskofu wa katoliki kwa kupiga marufuku michango

Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC, Twalib Mbarak ameipongeza hatua ya maaskofu wa kanisa Katoliki kupiga marufuku michango ya fedha nyingi makanisani, akisema itasaidia kukabili ufisadi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Twalib amesema hatua hiyo itasaidia katika kuwapo kwa uwazi na maadili.

Wakati uo huo, EACC imetoa wito kwa makanisa mengine kuiga mfano huo ili kupiga jeki vita dhidi ya ufisadi.

Hapo jana maaskofu hao walipiga marufuku yeyote anayetoa mchango wa zaidi ya shilingi elfu hamsini kanisani kwa mara moja.

Ikumbukwe Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki  limezindua kampeni ya kukabili ufisadi yenye kaulimbiu Kuvunja Ukimya Kuhusu Masuala ya Ufisadi wakati wa hafla ya maombi yaliyofanyika eneo la Subukia Kaunti ya Nakuru jana