array(0) { } Radio Maisha | Okoth awashauri wakazi kutoshawisjiwa na viongozi wa vyama vingine

Okoth awashauri wakazi kutoshawisjiwa na viongozi wa vyama vingine

Okoth awashauri wakazi kutoshawisjiwa na viongozi wa vyama vingine

Mgombea wa ubunge kupitia Chama cha ODM, katika Eneo Bunge la Kibra, Imran Okoth amewashauri wakazi kutokubali kushawishiwa na viongozi wa vyama vingine kuwapigia kura.

Akizungumza katika Kanisa la PCEA, Okoth amesema kuna baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiwapa pesa wakazi wa eneo hilo ili kuwapigia kura. Amesema wakazi hao ni watu wenye busara na watawachagua viongozi wanaopania kuwafanyia maendeleo.

Amewasihi kumchagua katika uchaguzi mdogo wa Novemba saba ili kuwawakilisha katika bunge.

Wakati uo huo, ameendelea kuwapongeza wakazi wa Kibra kwa kumchagua wakati wa mchujo, akisema kuna ishara kwamba yeye ndiye chaguo bora kwao