array(0) { } Radio Maisha | Afisa wa Polisi auliwa kwa kukatwakatwa kaunti ya Lamu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Afisa wa Polisi auliwa kwa kukatwakatwa kaunti ya Lamu

Afisa wa Polisi auliwa kwa kukatwakatwa kaunti ya Lamu
Mwili wa afisa wa Polisi aliyekuwa akihudumu Kaunti ya Lamu ambaye alitoweka katika njia tatanishi miezi miwili iliyopita umepatikana.
 
Mwili huo umepatikana  na majeraha huku ikikisiwa kuwa afisa huyo aliuliwa kwa kukatwakatwa huku mwili wake ukipatikana bila kichwa na mikono.
 
Mwili huo wa afisa wa cheo cha  costable, Hesbon Okemwa Anunda ulipatikana jana jioni kandokando ya barabara ya Kizingitini - Mbwachucini ndani ya kichaka.
 
Inaarifiwa Marehemu aliyekuwa akihuduMU kwenye Kituo cha Polisi cha Tchundwa huenda aliteswa kabla ya kuuliwa.
 
Taarifa iliyonakiliwa kwenye Kituo hicho cha Polisi inaonesha kwamba bunduki aina ya G3 na zaidi ya risasi sitini alizokuwa nazo mwendazake hazikupatikana ikiaminika huenda ziliibwa na waliotekelezwa unyama huo.
 
Kamishina wa Kaunti ya Lamu Perminus Kioi amesema kwamba uchunguzi unaendelezwa kufuatia mauwaji ya afisa huyo.
 
Mwili wa Okemwa umelazwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Mpeketoni.