array(0) { } Radio Maisha | Wafanyabiashara kufanya maombi maalum siku ya mashujaa

Wafanyabiashara kufanya maombi maalum siku ya mashujaa

Wafanyabiashara kufanya maombi maalum siku ya mashujaa

Huku shughuli ya kuitafuta mili ya watu wawili waliozama katika Kivuko cha Likoni Jumapili iliyopita ikiingia siku ya saba leo hii, Vuguvugu la Wafanyabiashara  katika eneo la Pwani limesema litafanya maombolezi maalum siku ya ya Mashujaa kwa katika eneo hilo.

Likiongozwa na Mwenyekiti wake Salim Karima vuguvugu hilo limesema kwamba litakongamana katika Uwanja wa Tononoka kwa maombolezi hayo.

Limeeleza kusitishwa na jinsi ambavyo hadi kufikia sasa mili ya Mariam Kigenda na mwanawe Amanda Mutheu ingali baharini.

Vuguvugu hilo limeilaumu Serikali kwa Utepetevu huku likiwashikiza wakazi wa Pwani kujitokeza kwa wingi kujuika nao kwa maombolezi hayo maalum.